INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Monday, November 9, 2015

Lulu Awambwatukia Wanaohoji Urembo Wake.

STAA asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacharukia watu wanaohoji kwa nini anapendeza angali mwanafunzi kwa kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni mwiko kupendeza?’
Akizungumza  na mwandishi wa habari hii hivi karibuni,  Lulu alisema amekuwa akiona maoni ya watu wengi mtandaoni wakihoji anapata wapi fedha za kupendeza wakati yeye ni mwanafunzi hoja ambayo ameiona haina mashiko kwani yeye hatumii fedha nyingi katika urembo wake.

“Watu bwana! Ningekuwa niko rafu wangesema pia na hata hivi ninavyopendeza watu wanachonga pia sasa jamani kipi kitu kizuri ili watu wafurahi na nafsi zao? Mimi umaridadi hapa ndiyo kwake na  sijaanza leo, japo sina fedha lakini kidogo nilichonacho kinaficha umasikini,” alisema Lulu.
Chanzo: GPL

No comments:

Post a Comment